JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
 
 
     
TEKNOHAMA
 
Teknohama [ Nyumbani ] au
 

 

 
ENG. SAMWEL T. DAUD
Mtaalamu wa ICT
Sekretarieti ya Mkoa
0754 4182 41
 
Utangulizi
 

Kwa kuzingatia umuhimu wa TEKNOHAMA na lengo la serikali la kuwa na serikali mtandao, Mkoa umeajiri mtalamu wa TEKNOHAMA kupitia programu ya serikali ya ISP.

TEKNOHAMA Mkoani Kagera ni ya kuridhisha kwa sasa,kwani huduma zote muhimu za simu na mtandao zinapatikana vizuri.

Kampuni kongwe ya TTCL ndio inayotoa huduma za mawasiliano ya njia ya simu katika ofisi nyingi za serikali na mashirika Mkoani Kagera.

Makampuni mengine ya simu za mkononi yametawanyika vizuri hadi katika baadhi ya vijiji na hivyo kufanya mawasiliano kuwa rahisi zaidi.

Hali hiyo imewasaidia wakulima kujua bei halali ya soko la mjini kwa mazao yao na hivyo kuondoa adha ya kuibiwa na wafanyabiashara kwa kisingizio kuwa soko la bidhaa husika ni mbaya.

 
 
 

 

 
 
 
SERIKALI-MTANDAO MKOANI.
 
 
 

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imejenga miundombinu ya TEKNOHAMA iliyo bora kwa ajili ya kuwa na serikali -mtandao.Aidha Ofisi nyingi hapa Mkoani hutumia teknolojia ya kompyuta katika kufanikisha shughuli za kila siku.

Halmashauri zote za Mkoa wa Kagera hazina miundombinu ya TEKNOHAMA iliyo bora hadi sasa isipokuwa Manispaa ya Bukoba.Juhudi nyingi zinafanywa ili kujenga miundombinu hiyo kabla ya mwaka 2013 kwa lengo la kuharakisha lengo la serikali la kuwa na Serikali -Mtandao.

 
MKONGO WA TAIFA
Mkongo wa Taifa ambao tayari umefika mkoani Kagera, umeweza kuongeza ufanisi wa huduma ya intaneti kwa kiwango kikubwa. Hadi sasa kampuni ya simu ya TTCL imeweza kutoa kutoa huduma bora zaidi za intaneti baada ya mkongo wa Taifa kuanza kufanya kazi hapa mkoani Kagera.
 
 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 
TELE-CENTERS
 

Mkoa una vituo viwili hadi sasa vinavyotoa huduma ya TEKNOHAMA vijijini. kituo kimoja kimoja kipo wilaya ya bukoba vijijini katika kijiji cha Kibegwe kata ya Bugabo, na kingine kipo katika wilaya ya Ngara.

Vituo hivyo vimekuwa vikitoa huduma nzuri kwa wanavijiji wa maeneo husika,ingawa vimekuwa havitoi huduma ipasavyo kutokana na mwamko duni wa wanavijiji katika matumizi ya TEKNOHAMA.

 
 
 
 
 

 

 

 
 
 
         
         
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 028-2752184