USHIRIKA
|
|
| |
| Mr.Juma Mokili |
| Afisa Ushirika..... |
| Sekretarieti ya Mkoa |
| |
|
| |
Utangulizi |
| |
Dira ya Sera ya Ushirika Tanzania ni “ kuunda vyama vya ushirika imara na endelevu vyenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya wanachama ya kiuchumi na kijamii ”. Katika kutekeleza Dira, Mkoa wa Kagera umehakikisha kwamba vyama vyote vinavyoandikishwa Mkoani, msingi wake ni wanachama na vinakuwa vyombo huru vya kiuchumi.
Hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2008, Mkoa wa Kagera unavyo Vyama vya Ushirika vilivyoandikishwa 578 vya aina mbalimbali. Hili ni ongezeko la asilimia 79 kutoka vyama 459 vilivyokuwa vimeandikishwa kufikia mwezi Disemba 2006. Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo vilivyoandikishwa katika kipindi hiki cha miaka miwili 2007/08 ni 135. Ongezeko hili limechangiwa na zoezi la uhamasishaji wananchi kujiunga na SACCOS ili kujikwamua kiuchumi linaloendeshwa na uongozi wa Serikali ya awamu ya nne.
|
| |
|
| |
Mkoa wa Kagera unavyo vyama vya Ushirika 578 vya aina mbalimbali. Vyama vya msingi 225 vina shughuli ya ukusanyaji na ununuzi wa mazao. Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) vipo 253. Vyama vya aina nyingine ni 100. |
| |
MPANGO WA SERIKALI WA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI
|
| |
Utekelezaji wa mpango wa serikali wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi awamu ya kwanza ulizinduliwa Mkoani Kagera tarehe 24/02/2007 . Mikopo iliyotolewa katika awamu hii ni kama ifuatavyo:-
SACCOS 5 zimepata mikopo ya jumla ya sh. 393,000,000/= milioni kupitia CRDB.
Wajasiriamali 793 (Wanawake 45 na Wanaume 748) wamepata mikopo ya jumla ya sh.bilioni 1.738 kupitia matawi mbalimbali ya NMB Mkoani Kagera.
CHANGAMOTO
Changamoto zilizojitokeza katika mpango huu ni:-
Wananchi waliofaidika na mpango zaidi ni wale waishio mjini kuliko wananchi wa vijijini.
Urasimu wa upatikanaji mikopo kwa kuzingatia taratibu za kibenki.
Elimu ya ujasiriamali na upatikanaji mikopo kupitia Benki ilichelewa kutolewa kwa wananchi.
Mikakati ya kupambana na changamoto hizi ni:-
Kuzinduliwa kwa awamu ya pili ya mpango wa uwezeshaji ambapo wananchi wa vijijini watapata mikopo kupitia Benki ya Posta, Benki ya wakulima ya ushirika (KFCB Ltd.) , SCCULT, PRIDE (T) , FINCA na SACCOS zenye mfumo wa kibenki.
Wananchi wa vijijini na mjini wameanza kupata Elimu ya Ujasiriamali na jinsi ya kupata mikopo ya uwezeshaji kupitia Timu za wawezeshaji za kata, wilaya na mkoa ambao wamepewa mafunzo na Benki kuu ya Tanzania (BOT) .
|
|
VYAMA VYA MSINGI NA VYAMA VIKUU |
| |
| |
Vyama vya msingi 126 vimeungana na kuunda Chama kikuu cha Kagera Co-operative Union (1990) Ltd; vyama 62 vimeunda Karagwe District Co-operative Union Ltd na vyama 36 kuunda Biharamulo Co-operative Union Ltd, Chama kikuu kingine ni Kagera Farmers Co-operative Bank Ltd ambacho wanachama wake wanatokana na vyama vya ushirika vilivyomo ndani ya Wilaya za Bukoba, Muleba na Manispaa ya Bukoba.
|
|
VYAMA VYA AKIBA NA MIKOPO (SACCOS) |
Mkoa unazo SACCOS 253 zenye wanachama 37,983 ambao wana mtaji wa Shilingi bilioni 3.131. Mikopo iliyokwisha tolewa ni Shilingi bilioni 5.654, kati ya hizo Shilingi Bilioni 2.970 zimekwisha rejeshwa. SACCOS hizi zimepata mikopo ya Shilingi bilioni 3.599 toka taasisi zinazokopesha fedha . Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa wakati huu vinajiendesha kibiashara, tofauti na mfumo kongwe ambapo vilikuwa vinajihusisha na utoaji wa huduma zaidi.
SACCOS kwa mfumo mpya huwapa wanachama wake bidhaa nyingi zaidi, zikiwemo hifadhi ya akiba. Mwanachama anaweza kuweka na kuchukua akiba yake saa za kazi, kuhifadhi amana na kupata mikopo yenye masharti nafuu. Mwelekeo ni vyama hivi kutoa huduma za Kibenki hasa maeneo ya vijijini ambapo hazipo. Katika kipindi cha kuanzia msimu wa 2007/08 hadi sasa, Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) vimefanya maendeleo yafuatayo:-
SACCOS zimeongezeka kutoka 115 hadi 265
Idadi ya wanachama imeongezeka kutoka 14,920 hadi 39,400 na kati ya hao 15,792 ni wanawake ambao ni sawa na asilimia 42 ya wanachama wote.
Thamani ya Hisa imeongezeka kutoka Shilingi 118,929,450/= kufikia Shilingi 1,914,349,700/=.
Amana za wanachama na wasio wanachama zimeongezeka kutoka Shilingi 93,360,000/= hadi Shilingi 952,665,650/=.
Jumla ya wanachama 29,093 wamepata mikopo yenye thamani ya Shilingi 5,654,249,428/= kati ya hizo Shilingi 2,970,523,118/= zimerejeshwa na zimebaki Shilingi 2,683,726,310/=.
|
| |
| |
| |
| |
| |
|
| |
|
| |
| |
| |
|
|
| VYAMA VYA USHIRIKA WA AINA NYINGINE |
| |
| |
Mkoa wa Kagera unavyo Vyama vya Ushirika wa aina nyingine vipatavyo 100 vilivyosajiliwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika. Vyama hivyo ni:-
Vyama Vikuu |
4 |
Vyama vya Wafugaji |
29 |
Vyama vya Wakulima |
21 |
Vyama vya Watoa Huduma |
19 |
Vyama vya Wavuvi |
13 |
Vyama vya Walaji (Consumer) |
6 |
Vyama vya nyumba |
4 |
Vyama vya Usafirishaji |
2 |
Vyama vya Viwanda |
1 |
Vyama vya Madini |
1 |
JUMLA |
100 |
Sekta ya Ushirika inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo:-
Wanachama kupoteza imani kwa vyama vyao vya Ushirika kwa kushindwa kukidhi mahitaji yao.
Kutokuwa na uwazi katika uendeshaji shughuli za vyama vya ushirika.
Viongozi na watendaji kujilimbikizia mamlaka ya maamuzi hivyo kuonekana ndio wamiliki wa chama cha ushirika.
Katika kupambana na changamoto hizo hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na:-
Kutoa elimu kwa wanachama ya kuwa chama ni mali yao, hivyo wana wajibu wa kusimamia uendeshaji wa shughuli zake na wao kutimiza wajibu wa uanachama.
Elimu ya kuwajasirisha kuhoji mambo yanayofanyika kinyume na taratibu za uendeshaji wa vyama vya ushirika. Tofauti na zamani, hivi sasa shughuli zinaendeshwa kwa uwazi, mikutano ya kisheria kufanyika na taarifa kutolewa.
Kubandika kwenye mbao za matangazo taarifa mbalimbali ikiwemo Taarifa ya fedha.
Kuchagua viongozi kwa kujaza fomu na muda wa uongozi kuwekwa bayana.
Watendaji hawana nafasi ya kujilimbikizia mamlaka ya maamuzi kwa kuwanyima wanachama haki zao kama wenye mali na wamiliki.
Katika kupambana na changamoto hizo hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na:-
|
Kutoa elimu kwa wanachama ya kuwa chama ni mali yao , hivyo wana wajibu wa kusimamia uendeshaji wa shughuli zake na wao kutimiza wajibu wa uanachama.
Elimu ya kuwajasirisha kuhoji mambo yanayofanyika kinyume na taratibu za uendeshaji wa vyama vya ushirika. Tofauti na zamani, hivi sasa shughuli zinaendeshwa kwa uwazi, mikutano ya kisheria kufanyika na taarifa kutolewa.
Kubandika kwenye mbao za matangazo taarifa mbalimbali ikiwemo Taarifa ya fedha.
Kuchaguwa viongozi kwa kujaza fomu na muda wa uongozi kuwekwa bayana.
Watendaji hawana nafasi ya kujilimbikizia mamlaka ya maamuzi kwa kuwanyima wanachama haki zao kama wenye mali na wamiliki. |
| |
| |
| |
| |
| |
| |
|
| |
| |
| |
|