• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Local Government Authority
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Farming Opprtunities
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

Katibu Tawala Mkoa wa Kagera CP Diwani Athuman Akifungua Mafunzo ya Mifumo Iliyoboreshwa Kwa Watumishi Kutoka Mikoa ya Kagera na Kigoma

Imewekwa : June 6th, 2018

Mikoa ya Kagera na Kigoma Yapata Mafunzo ya Mifumo Iliyoboreshwa Katika Usimamizi wa Fedha na Uhitaji wa Watumishi Katika Vituo

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Washirika  wa Maendeleo ambao ni Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) waendesha mafunzo ya siku  mbili mkoani Kagera kuhusu mfumo ya usimamizi wa fedha, mfumo wa kubaini mahitaji ya Watumishi ulioboreshwa kwa mikoa ya Kagera na Kigoma.

Mafunzo hayo yanahusu Mfumo wa usimamizi wa fedha za umma wa EPICOR toleo la 10.2 ambao umeboreshwa ili kuwezesha  ubadilishanaji wa taarifa na Mfumo wa Mipango na Bajeti wa PlanRep na ule  wa Uhasibu na kutoa taarifa za fedha za vituo vya kutolea huduma FFARS.

Aidha, mafunzo hayo yanalenga pia kupata mrejesho wa matokeo ya zoezi la kubaini mahitaji ya watumishi kwa kutumia Mifumo ya Workload Indicators of Staffing Need (WISN), na Priority and Optimization Analysis (POA) mifumo iliyorahisishwa katika matumizi na kuzingatia uzito wa kazi katika vituo vya kutolea huduma.

Akifungua mafunzo hayo Juni 4, 2018 katika Hoteli ya Bukoba ELCT  Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera CP Diwani Athuman aliwakumbusha washiriki wa mafunzo kuwa usimamizi wa fedha za Umma lazima unaendane na maboresho yanayoendelea ndani ya Serikali ambapo Halmashauri zote pamoja na vituo vyake vya kutolea huduma  zinatumia mifumo mingi zaidi ya Mfumo wa Epicor.

CP Athumani aliitaja mifumo hiyo kuwa ni Mfumo wa ukusanyaji wa Mapato (LGRCIS), Mfumo wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya, ambao unapokea mapato ya papo kwa papo (Cost Sharing) na kutunza taarifa za wagonjwa (GoT-HoMIS), Mfumo wa taarifa za kihasibu kwenye Vituo vya Kutolea huduma (FFARS) pamoja na mfumo ulioboreshwa wa kuandaa Mipango na Bajeti (PlanRep).

“Uwepo wa mifumo hiyo unapelekea uhitaji wa kuunganishwa mifumo hiyo ili iwe rahisi katika upatikanaji wa taarifa kwa ngazi zote na kwa wadau wengine wa maendeleo. Aidha, mafunzo hayo yatapunguza changamoto za utoaji taarifa hasa kutoka katika vituo vya kutolea huduma pamoja na kuunganisha taarifa hizo kwenye hesabu za Halmashauri, na  kutoa taarifa za utekelezaji wa mipango na bajeti kwa kuzingatia matumizi ya fedha yaliyofanyika.” Alisistiza CP Athuman.

Katika hutua nyingine Serikali inatarajia kuajiri katika Sekta ya Afya Watumishi wapya 7,680 (6,180 wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na 1,500 wa Wizara ya Afya) na mafunzo hayo ya siku mbili yamelenga kuziwezesha Halmashauri na Mikoa ili ziweze kutumia Mfumo wa WISN na POA iliyorahisishwa kusambaza watumishi wapya na katika kuomba watumishi wengine wapya.

Mafunzo hayo yaliwajumuisha watumiaji wa Mifumo ambao ni Waweka Hazina, Maafisa Usimamizi wa Fedha, Wahasibu, Maafisa TEHAMA, Afisa manunuzi na Wakaguzi wa Ndani. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) wakishirikiana na Wataalam kutoka Mradi wa PS3.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Darasa la VII Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Kwanza Mwaka 2019 Mkoani Kagera. December 21, 2018
  • Wanafunzi wa Darasa la VII Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Kwanza Mwaka 2018 Mkoani Kagera. December 20, 2018
  • Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT) January 30, 2018
  • Matokeo ya Mtihani Kidato cha Nne (CSEE) 2017 January 30, 2018
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awaasa Wajumbe wa Kamati Kuu CCM Mkoa Kuacha Malumbano na Migogoro Ili Chama Kiisimamie Serikali Kutekeleza Ilani

    February 21, 2019
  • Waziri Mkuu Awasili Mkoani Kagera na Kutoa Wito Kwa Wakandarasi Wazawa Kukamilisha Miradi Kwa Wakati Wanayopewa na Serikali Bila Visingizio

    February 20, 2019
  • Shughuli za Mahakama Mkoani Kagera Zafunguliwa Rasmi Mwaka 2019 Kesi ya Mauaji ya Mwanafunzi Spelius Eradius Yasikilizwa Kwa Mara ya Kwanza

    February 06, 2019
  • Uongozi wa Mkoa wa Kagera Waweka Mikakati ya Kuthibiti Utoroshwaji wa Madini ya Bati Wilayani Kyerwa Kuuzwa Nchi Jirani

    February 04, 2019
  • Tazama zote

Video

Mkoa wa Kagera Umejipanga Kufufua Zao la Chai na Kuwainua Wakulima.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Kaunta ya Wageni

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa