• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Local Government Authority
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Farming Opprtunities
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Habari

Kwaheri ya Kuonana Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mstaafu Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu

Imewekwa : August 7th, 2018

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu  mara baada ya kukamilisha  majukumu yake ya Ukuu wa Mkoa hapo Jumatatu  Agosti 6, 2018 kwa kukabidhi rasmi ofisi rasmi kwa mrithi wake Brigedia Jenerali  Marco E. Gaguti Jumanne  Agosti 7, 2018 ametuaga na kuondoka rasmi kwenda kupumzika  baada ya miaka 43 ya utumishi wa umma.

Baba Salum M. Kijuu kwaheri tunakutakia baraka, heri na fanaka na Mwenyezi Mungu  akujalie maisha marefu wewe pamoja na familia yako. Imani yetu Wanakagera ni kuwa kwa kila ulichotoa kwaajili yetu Mungu atakulipa zaidi.

Mhe. Kijuu ulikuwa mlezi hasa sisi watumishi wa ofisi yako ulituongoza kwa kutuelekeza na kutufundisha kazi tutakumbuka daima. Uliwahudumia wananchi wote kila mmoja kutokana au kulingana na shida yake na kuhakikisha ufuatiliaji unafanyika mpaka mhusika shida yake inatatuliwa.

Mhe. Kijuu Wazee wanaolelewa katika Kituo cha Kiilima Halmashauri ya Wilaya Bukoba watakumbuka sana kwani kila wakati uliwapa kipaumbele sana kuhakikisha makazi yao yanaboreshwa na wanapata chakula kadri ya mahitaji yao, kauli yako kila mara ulisema lazima tuwaenzi wazee wetu kwani walitumikia taifa letu kwa uzalendo na kuwa kila mmoja anaelekea uzeeni. Kwaheri Mzee Kijuu.

Siyo Kituo cha Kiilima tu bali na Nyumba ya Wazee iliyopo katika Parokia ya Kashozi Jimbo Katoriki la Bukoba ulielekeza jengo lao lijengwe upya mara baada ya kwenda na kuliona kuwa lilikuwa halifai tena wazee kuishi baada ya kuathiriwa vibaya na Tetemeko la Septemba 10, 2016. Hukujali jengo linamilikiwa na nani bali tu kwasababu wanaishi wazee. Utakumbukwa sana na Wazeehao Mhe. Kijuu.

Nakumbuka kila mara katika ziara zako za kutembelea walengwa au wanufaika wa TASAF Awamu ya Tatu  kila ulipomkuta mzee amefanya jambo la maendeleo kwa kutumia fedha za TASAFU ulitoa pochi yako na kumuongezeafedha  na ulitoa mifano katika hotuba zako kuwa wazee wanafanya vizuri sana kwa kuzitumia fedha za TASAF. Tutakumuka Mhe. Kijuu.

Mwisho,  uliyoyafanya ya kukumbuka ni mengi mno na si rahisi kuyataja yote na kuyamaliza bali tunakutakia mapumziko mema na sisi tunakuhaidi kuwa tutayaishi yale yote ulotuachia ili kukuenzi. Kweheri Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Kagera kutabaki kuwa Nyumbani Kwako.

Matangazo

  • Wanafunzi wa Darasa la VII Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Kwanza Mwaka 2019 Mkoani Kagera. December 21, 2018
  • Wanafunzi wa Darasa la VII Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Kwanza Mwaka 2018 Mkoani Kagera. December 20, 2018
  • Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT) January 30, 2018
  • Matokeo ya Mtihani Kidato cha Nne (CSEE) 2017 January 30, 2018
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awaasa Wajumbe wa Kamati Kuu CCM Mkoa Kuacha Malumbano na Migogoro Ili Chama Kiisimamie Serikali Kutekeleza Ilani

    February 21, 2019
  • Waziri Mkuu Awasili Mkoani Kagera na Kutoa Wito Kwa Wakandarasi Wazawa Kukamilisha Miradi Kwa Wakati Wanayopewa na Serikali Bila Visingizio

    February 20, 2019
  • Shughuli za Mahakama Mkoani Kagera Zafunguliwa Rasmi Mwaka 2019 Kesi ya Mauaji ya Mwanafunzi Spelius Eradius Yasikilizwa Kwa Mara ya Kwanza

    February 06, 2019
  • Uongozi wa Mkoa wa Kagera Waweka Mikakati ya Kuthibiti Utoroshwaji wa Madini ya Bati Wilayani Kyerwa Kuuzwa Nchi Jirani

    February 04, 2019
  • Tazama zote

Video

Mkoa wa Kagera Umejipanga Kufufua Zao la Chai na Kuwainua Wakulima.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Kaunta ya Wageni

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa