• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Waziri Lukuvi Ahamishia Wizara Yake Mkoani Kagera Kumaliza Kero za Wananchi Kupimiwa Ardhi na Kupata Hati

Imewekwa : March 24th, 2020

Akiongea na Watumishi wa Idara ya Ardhi Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Wakuu wa Wilaya  pamoja na viongozi wa Mkoa katika ziara ya siku moja Mkoani Kagera Machi 14, 2020 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesisitiza kuwa sasa Wizara yake inahamia Mkoani humo ili kumaliza kero za wananchi kuhusu ardhi.

“Gharama za kupata hati ya ardhi Mkoani Kagera zilikuwa kubwa mno kutokana na gharama ya kusafiri kwenda Mwanza kufuatilia hati ilikuwa kubwa kuliko gharama za kupata hati yenyewe jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma molari wa wananchi kupima ardhi zao ili wapate hati. Mhe. William Lukuvi.

Mhe. Lukuvi alisema kuwa ili kuhakikisha kero zote za ardhi zinakwisha tayari amewateua Kamishna Msaidizi wa Ardhi, Mkurugenzi wa Upimaji wa Ramani, Msajili wa Hati, Mthamini pamoja na Maafisa wao ili kuhakikisha wananchi wanapata hati  mkoani Kagera badala ya kusafiri kwenda kuzifuata Mwanza na nyaraka za hati za Wananchi 16,000 ambao wamepima ardhi zao zilizokuwa Mwanza alisema zitahamishiwa Kagera.

Katika Kikao hicho Mhe. Lukuvi alisema kuwa mwishoni mwa mwezi huu Machi 2020 Wizara yake inahamia rasmi Mkoani Kagera ili kumaliza kero za muda mrefu kuhusu upatikanaji wa hati za ardhi za wananchi. “Kuwa na ardhi isiyopimwa hata kama umejenga jengo lenye thamani kubwa unakuwa na mali mfu lazima tupange na kuzipima ardhi za wananchi.” Alisistiza Mhe. Lukuvi

Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi aliwakumbusha Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuwa mamlaka ya upangaji wa ardhi ni jukumu na si jukumu la Waziri. “Pangeni ardhi zenu kwa matumizi sahihi na kuwamilikisha wananchi, nawaletea watendaji haya ni matrekta mapya yatumieni ipasavyo hata maeneo ya vijiji yanayoonekana kukua yapimeni na kuwapa wananchi hati.” Alipigilia msumali Mhe. Lukuvi

MwishoWaziri Lukuvi  alisistiza juu ya wananchi kupata hati katika Halimashauri zao bila kusafiri kufuatilia hati hizo ambapo aisema kuwa kama ni mwananchi wa Wilaya ya Ngara atapata hati yake hukohuko Ngara .

Pia upatikanaji wa hati katika mkoa utapunguza na kero kwa taasisi za kibenki kwa wateja wao wanaokopa kutumia hati hizo kwani walikuwa wanalazimika kusafiri kwenda Mwanza kuthibitisha. Ofisi za Wataalam wote wa Idara ya ardhi zitakuwa katika majengo ya ofisi za Mkuu wa Mkoa Kagera.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ziara ya Rais Magufuli Mkoani Kagera Yatoa Mwangaza na Njia ya Kukuza Uchumi wa Mkoa na Taifa la Tanzania

    January 23, 2021
  • Wakuu wa Mikoa ya Kagera na Mtwara Watembelea Miradi Mikubwa Inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano Mkoani Dar es Salaam.

    December 19, 2020
  • Meli ya New Victoria Yatia Nanga Katika Bandari ya Bukoba Wananchi Wajitokeza Kwa Wingi Kuipokea Meli Yao

    June 28, 2020
  • Msimu wa Kahawa Kagera Wafunguliwa Rasmi Wakulima Kulipwa Ndani ya Saa 48 Serikali Kusimamia Haki Zao

    June 09, 2020
  • Tazama zote

Video

Mkuu wa Mkoa wa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti Akimkaribisha Rais Magufu Mkoani Kagera Katika Ziara ya Siku Mbili Januari 18-19, 2021
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa