- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera una Jumla ya shule za Sekondari 251, kati ya hizo 191 ni za Serikali na 60 zinamilikiwa na Mashirika pamoja na watu binafsi. Shule za Sekondari za Serikali zenye madarasa ya kidato cha Tano na Sita (A - Level) zimeongezeka kutoka 12 mwaka 2010 hadi kufikia 21 mwaka 2017. Shule zilizoongezeka mwaka 2016/2017 ni 4 (Shule ya Sekondari Nyailigamba iliyopo Muleba, Murusagamba iliyopo Ngara, Kagemu na Omumwani zilizopopo Manispaa ya Bukoba).
Kwa upande wa Sekondari, ufaulu wa kidato cha pili Mkoa umepanda kutoka nafasi ya 12 mwaka 2015 na kuwa wa 4 kitaifa, na mtihani wa kidato cha Nne 2016 Mkoa wa Kagera umepanda hadi nafasi ya 3 kutoka nafasi ya 12 mwaka 2015. Wanafunzi waliofanya mtihani ni 13,800 na waliofaulu ni 11,241 na kupata GPA ya 3.8569 kati ya mikoa 30, kwa upande wa kidato cha sita, ufaulu umepanda kutoka nafasi ya 20 mwaka 2015 hadi nafasi ya 8 mwaka 2016.
Idadi ya Walimu Shule za Sekondari : Mkoa una jumla ya walimu wa Shule za Sekondari 3631 ambapo miongoni mwao 2281 ni wa kiume na 1350 ni wa kike kati ya 4126 wanaohitajika, ambapo walimu 1343 ni wa masomo ya sayansi kati ya 1797, hivyo kuna upungufu wa walimu 454 wa sayansi, na walimu 2288 ni wa masomo ya sanaa kati ya 2329 wanaohitajika, hivyo kuna upungufu wa walimu 41.
Hali ya Maabara za Sayansi katika Shule za Sekondari: Katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya sayansi katika shule za Sekondari, jumla ya vyumba vya maabara 573 vinahitajika, vyumba vinavyoendelea kujengwa ni 136, vyumba vilivyokamilika bila samani na fittings ni 220 na vyumba vilivyokamilika vyenye samani na vifaa vya kufundishia ni 217. Hii ni sawa na 37.87% ya ukamilishaji.
Miundombinuna Samani za Shule za Sekondari: Mkoa una jumla ya vyumba vya madarasa 1,918 sawa na asilimia 74 ya mahitaji, nyumba za walimu 500 kati ya nyumba 4,126 zinazohitajika na majengo ya utawala 160, kati ya majengo 190 yanayohitaji na Maktaba 175, kati ya 190 zinazohitajika.
Hali ya Madawati: Mkoa mzima una jumla ya madawati 273,484,kati ya madawati 272,150 yaliyohitajika kwa Shule za Msingi na Sekondari, Shule za Msingi wana madawati 201,359 kati ya madawati 200,045 yaliyohitajika, na Shule za Sekondari zina jumla ya madawati 72,125 kati ya 72,105 yaliyohitajika.
Rasilimali Watu Katika Shule za Sekondari za Serikali hadi Mwaka 2016: Mkoa wa Kagera una jumla ya walimu 13,304 wa shule za msingi na sekondari kati ya walimu 19,407 wanaohitajika ambapo kuna upungufu wa walimu 6,114 kwa Shule za Msingi na Sekondari. Kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali tatizo la upungufu wa walimu limepungua kwa kiasi kikubwa kwa mfano kwa mwaka 2015/2016 tu, jumla ya walimu 1,424 walipangiwa kazi katika Mkoa wa Kagera ingawa ni walimu 1,341 sawa na asilimia 94 walioripoti na kupangiwa vituo vya kazi. Pia mkoa wetu umepangiwa walimu 154 wa Sayansi, walimu 143 wameripoti hadi kufikia 27 Aprili 2017 na walimu 11 hawakuripoti.
Hali ya Walimu wa Masomo ya Sayansi Katika Shule za Sekondari Mkoa wa Kagera: Walimu wa masomo ya sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia na Hisabati) ni kama ifuatavyo;- Somo la Hisabati walimu waliopo 218 sawa na 40% kati ya 542 wanaohitajika sawa na asilimia 31. Somo la Fizikia walimu waliopo ni 169 sawa na 37% kati ya walimu 453 wanaohitajika sawa na asilimia 26. Somo la Kemia waliopo ni 214 sawa na 47% kati ya 457 wanaohitajika sawa na asilimia 36 na Somo la Baiolojia walimu waliopo ni 228 sawa na 49% kati ya 468 wanaohitajika sawa na asilimia 38.
Utekelezaji wa Elimu Bila Malipo: Katika kuzingatia dhana ya Elimu bila malipo, kwa kipindi cha mwezi Januari 2016 hadi Juni 2017, Mkoa umepokea jumla ya Tshs. 9,945,542,551/= kugharimia uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari pasipo wazazi/walezi kulipa ada wala michango.
Ujenzi wa Shule za Kidato cha Tano na Sita: Mkoa una mpango wa kujenga angalau shule 2 kila Halmashauri za kidato cha tano na sita. Halmashauri za Ngara na Muleba wanakamilisha ujenzi na Halmashauri za Missenyi, Bukoba, Bukoba Manispaa, Karagwe, Biharamulo na Kyerwa zimebainisha shule hizo na ujenzi unaendelea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa