Mkoa wa Kagera una Vyuo vya Ualimu 3, ambapo kati ya vyuo hivyo cha serikali ni 1 na visivyo vya Serikali ni 2. Vyuo hivyo ni St Francis Nkindo TTC na King Rumanyika TTC. Hivi ni vyuo vya watu binafsi na viko Wilaya ya Bukoba. Chuo cha Ualimu Katoke ni chuo pekee cha Serikali kilichoko Wilayani Muleba.
Pia tuna Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Vyuo vya Ufundi vipo 22 na vyuo vikuu 3 ambavyo ni Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Josiah Kibira na chuo kikuu kishiriki cha Mt. Augustino (KARUMCO). Hata hivyo vyuo vikuu vya Josiah Kibira na Mtakatifu Augustino vimefungiwa kudahili wanafunzi kwa kupungukiwa na sifa. Vyuo hivyo vinaendelea kukamilisha sifa zinazotakiwa ili viweze kuruhusiwa kuendelea kudahili wanafunzi.