|
![]() |
|
|
Mhe. Julieth Nkembanyi Binyura
|
|
|
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe
|
|
|
![]() |
|
|
Bw. Innocent M. Nsena
|
|
|
Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe
|
|
WASIFU WA KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KARAGWE BWANA INNOCENT MAHENDEKA NSENA
Na.
|
AINA YA TAARIFA
|
MAELEZO
|
|||||
1. |
JINA KAMILI NA UTAMBULISHO
|
Innocent Mahendeka Nsena (Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe)
|
|||||
2. |
TAREHE YA KUZALIWA
|
6 Juni, 1974
|
|||||
3. |
ELIMU AU MAFUNZO
|
JINA LA SHULE/CHUO
|
KUTOKA MWAKA |
HADI MWAKA |
KIWANGO (MFANO CHETI/SHAHADA)
|
||
(i) |
Stadi ya Masuala ya Jamii
|
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Kivukoni)
|
2008 |
2010 |
Stashahada
|
||
(ii) |
Siasa na Usimamizi wa Maendeleo ya Jamii
|
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Kivukoni)
|
2010 |
2013 |
Shahada
|
||
(iii) |
Utawala wa Umma
|
Chuo Kikuu Mzumbe
|
2013 |
2015 |
Shahada ya Uzamili
|
||
4.
|
UZOEFU NA AJIRA
|
KAMPUNI/TAASISI |
NAFASI
|
KUTOKA MWAKA |
HADI MWAKA |
||
(i) |
Katibu Tawala
|
Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera
|
Katibu Tawala wa Wilaya
|
2017 |
Hadi Sasa |
||
(ii) |
Mkuu wa Utawala
|
Chama Cha Mapinduzi
|
Mkuu wa Utawala Makao Makuu
|
2016 |
2016 |
||
(iii) |
Katibu Msaidizi wa Mhasibu
|
Chama Cha Mapinduzi
|
Katibu Msaidizi Mhasibu (W)
|
2016 |
2016 |
||
(iv) |
Katibu wa Umoja wa Vijana
|
Umoja wa Vijana wa CCM
|
Katibu UVCCM
|
2005 |
2005 |
||
(v) |
Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya Kusanyiko la Wahitimu wa Vyuo VIkuu
|
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
|
Mwenyekiti
|
2010 |
Hadi Sasa |
||
(vi) |
Mjumbe wa Bodi ya Ushauri Shule ya Sekondari Lugongo
|
Shule ya Sekondari Lugongo
|
Mjumbe wa Bodi
|
2007 |
2010 |
||
(vii) |
Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza
|
Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza
|
Mjumbe wa Bodi
|
2007 |
2013 |
||
5. |
UZOEFU KATIKA SIASA
|
CHAMA |
NAFASI |
KUTOKA MWAKA |
HADI MWAKA |
||
(i) |
Mjumbe Mkutano mkuu wa CCM Taifa
|
Chama cha Mapinduzi
|
Mjumbe |
2008 |
2012 |
||
(ii) |
Katibu wa CCM Tawi la Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
|
Chama cha Mapinduzi
|
Katibu |
2009 |
2010 |
||
(iii) |
Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Mkoa
|
Umoja wa Vijana wa CCM
|
Mjumbe |
2004 |
2009 |
||
(iv) |
Mjumbe Baraza Kuu la UVCCM Wilaya
|
Umoja wa Vijana wa CCM
|
Mjumbe |
2004 |
2009 |
||
(v) |
Mjumbe Kamati ya YUtekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Wilaya
|
Umoja wa Vijana wa CCM
|
Mjumbe |
2004 |
2009 |
||
|
|
|
|
|
|
|
|
HISTORIA YA WILAYA YA KARAGWE |
CHIMBUKO LA KARAGWE NA WATU WAKE (WANYAMBO)
|
Jina " Karagwe " kutokana na simulizi za wazee wetu mbali mbali na watafiti wa historia ya Karagwe kama ( Katoke 1975; 162) inaelezwa kwamba jina hili linatokana na kilima kinachopatikana Kusini Magharibi ya Makao makuu ya wilaya ya Karagwe ,kwenye kijiji cha Kandegesho ,kata ya Nyakakika ambacho mtawala (Omukama) wa kwanza alifanya kafara ya kwanza. Taarifa zilizopo mtawala huyo alijulikana kwa jina la Nono ya Malija kutoka ukoo wa Basiita. Na kwamba kumbukumbu hii ya "Karagwe ka Nono "inatokana na ukweli kuwa Nono alikuwa mtawala wa mwisho wa wenyeji asilia kabla ya kuondolewa madarakani na Omukama Ruhinda mtoto wa Wamara. Inasemekana kwamba Nono aliondolewa kwa ujanja bila ya misukosuko wala mapigano ya aina yoyote. Kwa kifupi hii ndio kumbukumbu yake na chimbuko la historia ya jina Karagwe.
MIPAKA YA WILAYA
|
Wilaya ya Karagwe ni kati ya Wilaya saba (7) za Mkoa wa Kagera. Wilaya inapakana na Wilaya ya Kyerwa upande wa Kaskazini, Nchi ya Rwanda upande wa Kusini Magharibi, Wilaya ya Ngara upande wa Kusini na Wilaya za Missenyi, Bukoba Vijijini na Muleba upande wa Mashariki.
JIOGRAFIA YA WILAYA
|
Wilaya ipo kilomita 115 kutoka Manispaa ya Bukoba –Makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Wilaya inapatikana kati ya nyuzi 1o na 2o, 20' Kusini Latitudo 30o hadi 38,30 Mashariki Longitudo. Mwinuko wa ardhi kutoka usawa wa bahari ni mita 1,500 hadi mita 1,800. Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la wastani wa degree 26oC. Mvua zinanyesha kwa wastani wa mm 1,040 hadi 1,200 kwa mwaka, kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na mwezi Mei.
ENEO LA WILAYA
|
Wilaya ya Karagwe ina eneo la kilomita za mraba 4,500 kati ya hizo kilomita za mraba 4,342 ni eneo la nchi kavu na kilomita za mraba 158 ni eneo la maji. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 153,540 na eneo linalolimwa ni Hekta 82,808.5 sawa na asilimia 53.9.
UTAWALA
|
Maeneo ya Utawala yamebadilika kutoka Tarafa 4, Kata 28, Vijiji 109 na Vitongoji 1,162 mwaka 2005 hadi Tarafa 5, Kata 23, Vijiji 77 na Vitongoji 629 mwaka 2014. Vitongoji 594 vipo katika Halmashauri ya Wilaya na vitongoji 35 vipo katika Mamlaka ya mji mdogo. Waheshimiwa Madiwani wa kuchaguliwa wapo 23 na Waheshimiwa Madiwani Wanawake Viti maalum 7.
IDADI YA WATU
|
Kulingana na Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Karagwe ilikuwa na jumla ya watu wapato 332, 020. Kati ya hao 163,864 (wanaume) na 168,156 (wanawake), ambapo ongezeko la watu ni asilimia 2.9 kwa mwaka.
Maoteo ya watu kwa mwaka 2015 ni kuwa Wilaya ilikuwa na watu 351,555. Kati ya hao, wanawake ni 178,050 na wanaume ni 173,505. Aidha idadi ya kaya nayo imeongezeka toka kaya 72,836 mwaka 2012 hadi kaya 76,425 mwaka 2015.
ORODHA YA WAKUU WA WILAYA YA KARAGWE TANGU MWAKA 1961 HADI SASA |
NA.
|
JINA KAMILI
|
MWAKA WA KUINGIA |
MWAKA WA KUTOKA |
21.
|
NDG. JULIETH NKEMBANYI BINYURA |
2021
|
-
|
20. |
NDG. GODFREY A. MHELUKA
|
2016 |
2021 |
19. |
NDG. DEODATUS L. KINAWILO
|
2015 |
2016 |
18. |
NDG. DARRY I. RWEGASIRA
|
2012 |
2015 |
17. |
NDG. ISSA S NJIKU (AG)
|
2011 |
2012 |
16. |
NDG. FABIAN I. MASSAWE
|
2009 |
2011 |
15. |
NDG. FRANK UHAHULA
|
2006 |
2009 |
14. |
NDG. DAVID J. DAUD
|
2004 |
2004 |
13. |
NDG. SANING’O OLE TELELE
|
2000 |
2004 |
12. |
NDG. PETER KANGWA
|
1999 |
2000 |
11. |
NDG. GERARD J. GHACHOCHA
|
1997 |
1999 |
10. |
NDG. JOSEPH E. NDITI
|
1994 |
1997 |
09. |
NDG. LUHOZYO E. SIWALE
|
1989 |
1994 |
08. |
NDG. MOHAMED CHIMSALA
|
1984 |
1989 |
07. |
NDG. RAPHAEL CHAYAKO
|
1980 |
1984 |
06. |
NDG. F.X. ITALA
|
1978 |
1980 |
05. |
NDG. RUHASI
|
1977 |
1978 |
04. |
NDG. THOMAS MSONGE
|
1973 |
1977 |
03. |
NDG. LOSA LIYEMBA
|
1969 |
1973 |
02. |
NDG.ENOS RYANGARO
|
1965 |
1969 |
01. |
NDG. PETER N. KAFANABO
|
1961 |
1963 |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa